Home Habari za michezo DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI…MBRAZILI ASHINDWA KUJIZUIA NA TABIA ZA INONGA…

DAKIKA KADHAA KABLA YA MECHI…MBRAZILI ASHINDWA KUJIZUIA NA TABIA ZA INONGA…

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema anafurahishwa na ushirikiano uliopo kwenye safu yake ya ulinzi inayoongozwa na Beki kutoka DR Congo Henock Inonga.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo, huku kikosi chake kikiwa katika maandalizi ya kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa watetezi Wydad AC, utakaopigwa leo Ijumaa (Aprili 28) saa nne usiku kwa saa za Tanzania.

Robertinho amesema pamoja na kufurahishwa na uwezo wa Inonga, pia anapenezwa na uchezaji wa mabeki wengine kama Mohamed Hussein, Kapombe, (Shomari) na Josha Onyango.

“Unaona kwenye upande wa ulinzi ninafurahishwa na namna wanavofanya kazi, mtazame Mohamed Hussein, Kapombe, (Shomari), Inonga (Henock) kila mmoja anafanya kazi kwa kujituma.

“Wote wanashirikiana na hii inaongeza nguvu kwenye eneo hilo kwani ili ushinde ni lazima uhakikishe kwamba haufungwi, hili ni jambo la msingi na tunalifanyia kazi kila wakati,” amesema kocha huyo mwenye umri wa miaka 62

Inonga ambaye anashirikiana na Joash Onyango, jina lake limepenya kwenye kikosi bora cha CAF cha juma hili baada ya kumalizika michezo ya Mkondo wa Kwanza ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  MAKAMBO NA YANGA IMEISHA, ISHU YA MORRISON YAIBUKA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO