Home Habari za michezo HIZI HAPA SIKU 109 ZA MBRAZILI NDANI YA SIMBA SC….WALIOSEMA HAWEZI WAKIMBIA...

HIZI HAPA SIKU 109 ZA MBRAZILI NDANI YA SIMBA SC….WALIOSEMA HAWEZI WAKIMBIA KIMYA KIMYA…

Kocha Mkuu Simba SC

Leo Aprili 22 Kocha Mkuu wa Simba SC Robert Olivieira ‘Robertinho amefikisha siku 109 akiwa ndani ya klabu hiyo tangu apewe ajira na kutangazwa Januari 3,2023.

Wakati anafika na hata alipoanza kazi hakuonekana kama kukubalika zaidi ndani ya klabu hiyo, lakini ndani ya mwendo wa kazi zake tayari ameshaanza kujiwekea mizizi akifanikiwa kuibadilisha timu yake na kuanza kupita njia za matarajio ya kikosi hicho.

Kuna alama ambazo Robertinho raia wa Brazil ameanza kuzionyesha ndani ya kikosi chake na haya yafuatayo ni mambo ambayo yamempa mafanikio akiwa ndani ya mwezi wa nne wa ajira yake.

KUFUZU ROBO FAINALI CAF

ZA NDANI KABISA...RASMI RONALDINHO APEWA RUNGU SIMBA...KIGOGO MSIMBAZI AFUNGUKA HAYAWakati anatua Simba SC aliikuta tayari imeshatinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akipokea kazi nzuri ya aliyekuwa kocha wa muda, Juma Mgunda ambaye sasa ni msaidizi wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho.

Kwenye mechi 6 ambazo Simba SC ilicheza hatua ya makundi Robertinho amefanikiwa kuipeleka hatua ya robo fainali na sasa watacheza na bingwa mtetezi Wydad Athletic ya Morocco, Jumamosi Aprili 22, haya ni mafanikio ambayo yatampa heshima kocha huyo bila kujali matokeo yajayo dhidi ya vigogo hao.

Endapo Robertinho atawafunga Wydad basi atakuwa ameupiga mwingi ambao utamfanya kuheshimika zaidi lakini hata kama atapoteza na kutolewa bado atabaki salama kwa hatua ambayo ameifikisha Simba.

CHAMA KUINGIA KATIKA MFUMO

Habari za SimbaKama kuna tukio ambalo lilitishia maisha ya Robertinho Simba ni Januari 18,2023 Simba ikicheza nyumbani dhidi ya Mbeya City na ndani ya dakika 30 akamtoa kiungo fundi Clatous Chama na kumuingiza winga Pape Sakho.

Mabadiliko yale hayakupokelewa vizuri na mashabiki wa Simba wakiona kama kocha wao mpya anaivuruga timu na kibaya zaidi baada ya kiungo huyo kutolewa alikuwa ameshatengeneza bao la kwanza na alipotolewa wageni wakasazisha.

Hata hivyo, Sakho aliyeingia alimbeba Robertinho kwa kufunga bao safi la kideoni dakika ya 55 hatua ambayo kiasi fulani liliwatuliza mashabiki.

Kocha huyo kuna vitu alikuwa anataka vibadilike kwa Chama kwa kumtaka kiungo huyo kuwa na msaada kwa wenzake hasa timu inapopoteza mpira mabadiliko ambayo sasa yamemuongezea sio tu ubora Chama bali hata wachezaji wengi kubadilika wakiwa wanakaba na kushambulia kwa kasi.

USHINDI WA YANGA

Habari za Simba SCTakribani misimu mitatu Simba ilikuwa haijawafunga watani wao wa jadi Yanga, mara ya mwisho wekundu hao kushinda ilikuwa mwaka 2019.

Simba chini ya Robertinho ikapindua meza wikiendi iliyopita Aprili 16 baada ya kuwachapa Yanga kwa mabao 2-0 tena ukiwa mchezo muhimu wa ligi ambao endapo Yanga ingeshinda ilikuwa inakwenda kuyatumia matokeo hayo ya mechi ya watani kurahisisha safari ya kuchukua ubingwa wa pili mfululizo.

Matokeo haya yaliendelea kumbeba Robertinho Simba kwa kuifunga Yanga ambayo ilikuwa inaonekana kuwa na kikosi bora kushinda cha wekundu hao.

HAJAPOTEZA LIGI KUU

Habari za Simba SCKama hufahamu ni kwamba Robertinho ambaye ni winga wa zamani wa Brazil ameiongoza Simba katika jumla ya mechi 14 za mashindano yote na katika hizo 7 ni za ligi kuu bara na hajawahi kupoteza mechi yoyote.

Amefanikiwa kushinda mechi 6 na kutoa sare moja kwenye ligi akiwa hajapoteza mechi yoyote lakini pia ameshinda mechi moja ya Kombe la Azam Shirikisho dhidi ya Ihefu.

Kimataifa ameiongoza Simba kwenye mechi 6 za Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi akishinda 3 na kupoteza 3 lakini kikosi chake kikaweka rekodi ya kuwa timu iliyopata ushindi mkubwa katika hatua hiyo kupitia matokeo ya kuwachapa Horoya AC ya Guinea mabao 7-0 nyumbani wakifuatiwa na Raja ambao waliichapa Vipers kwa mabao 5-0 huku Mamelodi Sundowns wakishika nafasi ya tatu baada ya ushindi wao wa mabao 5-2 dhidi ya Al Ahly.

SIMBA INABADILIKA

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA...HAWA HAPA MAREFA WA MCHEZO HUOSimba chini ya Robertinho inaendelea kupigania heshima ya klabu hiyo licha ya changamoto za ubora wa wachezaji ambazo zilikuwa zinaonekana kabla, Robertinho ameifanya timu hiyo kuruhusu mabao manne tu kwenye ligi lakini ikifunga 15.

Kimataifa Simba ilifanikiwa kufunga mabao 10 yakiwemo mawili waliyofunga katika ushindi pekee wa ugenini dhidi ya Vipers na lingine likiwa la kufutia machozi walipopoteza ugenini dhidi ya Raja kwa mabao 3-1 lakini pia wakiruhusu mabao 6 katika mechi 6.

BADO YUMO NJIA YA MATAJI

SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD...VAR ITATUMIKA...MANULA,KANOUTE OUTKimahesabu huwezi kumuondoa Simba katika mataji matatu, ikiwa bado inaikimbiza Yanga ambao wanaongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 5 baada ya kushinda wikiendi iliyopita Robertinho alipunguza pengo hilo kwa alama tatu kutoka 8 za awali.

Simba pia bado inalitaka taji la Kombe la Azam Shirikisho wakiwa tayari wanasubiri mechi ya nusu fainali wakikutana na Azam ili watinge fainali lakini pia bado wapo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wakikutana na bingwa mtetezi hatua ambayo inaendelea kumlinda kocha huyo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUWAFUNGA MARA 2 WARUSI JANA....KIYOMBO AFUNGUKA ALICHOAMBIWA NA 'MZUNGU'..