Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU DILI LA KINZUBI KUTUA YANGA…GSM AACHA BALAA KWA...

HUU HAPA UKWELI KUHUSU DILI LA KINZUBI KUTUA YANGA…GSM AACHA BALAA KWA KATUMBI..

Habari za Yanga

Mpaka sasa unaweza kusema winga wa TP Mazembe, Philippe Kinzumbi mambo yake na Yanga yapo safi kwani kuna uwezekano mkubwa dili lake la kutua kikosini hapo likakamilika nchini DR Congo.

Hiyo ni baada ya awali winga huyo raia wa DR Congo kubainisha wazi kwamba anatamani kujiunga na Yanga kama watakuwa wanahitaji huduma yake.

Licha ya TP Mazembe kushindwa kufanya vema katika michezo ya kimataifa msimu huu na kufeli kufuzu Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yeye amekuwa akionesha kiwango bora, huku akitoa pasi tatu za mabao katika michuano hiyo.

Yanga wameonekana kuvutiwa na huduma ya wiga huyo, huku taarifa za ndani kutoka klabuni hapo, tumezipata ni kuwa huenda Yanga wakatumia nafasi ya kwenda DR Congo kumalizana na mchezaji huyo kulingana na uwezo wa kukutana na viongozi wa pande zote mbili kuwa mkubwa.

“Yanga wanaweza kuitumia nafasi ya kucheza na TP Mazembe kukamilisha vitu viwili vikubwa ambavyo vimewapeleka DR Congo. Cha kwanza wanaweza kukamilisha ishu ya kushinda kwani wanataka kumaliza vinara wa Kundi D, lakini cha pili wanataka kukamilisha jambo la usajili wa Kinzumbi kutoka TP Mazembe.

“Kama ambavyo unafahamu, Kinzumbi amekuwa ni mchezaji mzuri kwa muda mrefu na Yanga walimuulizia baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa Dar, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mazungumzo mengine kuendelea DR Congo kwa kuwa Yanga watakutana na uongozi wa timu na uongozi unaomsimamia mchezaji husika,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  KISA KUPOTEZA UBINGWA WA MAPINDUZI..NABI AFURA KWA HASIRA YANGA...ATOA AMRI HII MPYA...