Home Habari za michezo MKUDE AZIDI KUPOTEANA SIMBA….HIZI HAPA TAKWIMU ZAKE KWA MSIMU HUU TU…

MKUDE AZIDI KUPOTEANA SIMBA….HIZI HAPA TAKWIMU ZAKE KWA MSIMU HUU TU…

Habari za Simba

Anaupiga mwingi uwanjani lakini kama msimu huu kwake kuna tatizo kutokana na kupata nafasi kiduchu ya kuonyesha yale makeke yake ndani ya uwanja.

Amepewa jina la Nungunungu akifanishwa na yule mnyama mdogo lakini ana miba mwili mzima kiasi kwamba huwezi kumgusa kirahisi.

Ni Jonas Mkude, kiungo wa Simba ambaye msimu huu ameutumia nje ya uwanja kuliko ndani kutokana na kusepa na dakika kiduchu kitaifa na kimataifa. Hapa tupo naye kwenye mwendo wa data namna hii;

Mechi zake za ligi ni nane akiyeyusha dakika 593 kwenye mechi za kimataifa wakati Simba ikitinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kacheza mechi mbili akisepa na dakika 48.

Hivyo kwenye mechi za mashindano ikiwa ni ligi ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ni mechi mbili kacheza akisepa na dakika 641.

KATUPIA MOJA, PASI MOJA YA BAO Mwamba katupia bao moja dakika ya 85 ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa na ana pasi moja ya bao kibindoni alitoa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkapa dakika ya 44.

Alivuja jasho hivi; SIMBA 3-0 GEITA GOLD ALIYEYUSHA DAKIKA 35 ALICHEZA FAULO 2. Tanzania Prisons 0-1 Simba aliyeyusha dakika 90 alipachika bao moja. Simba 3-0 Dodoma Jiji, dakika 90 alicheza faulo dakika ya 9 na mwamuzi wa kati alikuwa ni Ramadhan Kayoko.

Yanga 1-1 Simba, alisepa na dakika 90 alicheza faulo dakika ya 8 alichezewa faulo dakika ya 21 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 31, Uwanja wa Mkapa.

Azam FC 1-0 Simba alisepa na dakika 73 akishuhudia timu hiyo ikiyeyusha pointi tatu mazima.

Simba 5-0 Mtibwa Sugar alisepa na dakika 80 alicheza faulo dakika ya 37 alipiga faulo dakika ya 10,55.

Singida Big Stars 1-1 Simba alisepa na dakika 45, Uwanja wa Liti Mbeya City 1-1 Simba, Uwanja wa Sokoine alisepa na dakika 90 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 40,alicheza faulo dakika ya 26,34.

VIWANJA Kwenye mechi 8 za ligi Mkude kacheza mechi sita Uwanja wa Mkapa, mbili Uwanja wa Sokoine na moja Uwanja wa Liti. Zile za kimataifa zote mbili kakiwasha Uwanja wa Mkapa.

KIMATAIFA Simba 1-0 de Agosto alisepa na dakika 3 Uwanja wa Mkapa. Simba 0-3 Raja Casablanca, dakika 45 Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  MECHI YA AZAM VS GOR MAHIA YAPEPERUKA ISHU IKO HIVI