Habari za michezo
RASMI YANGA KUKUTANA NA WABABE HAWA…NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO
Marce Ben Komba
May 1, 2023
7:56 am
Timu ya Yanga imeweka rekodi baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Hatua hiyo imekuja baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Mkapa mchezo wa mkondo wa pili wa Robo Fanali dhidi ya Rivers United kutoka Nigeria.
Yanga wanaingia hatua ya Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0 walioupata ugenini katika mchezo wa Mkondo wa kwanza.
Yanga kwa sasa inakwenda kukutana na Marumo Gallants ya Afrika ya Kusini katika Mchezo wa Nusu Fainali, baada ya kufanikiwa
kuiondoa Pyramids ya Misri.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.