Habari za Simba SC
Habari za michezo

ZIMBWE JR AZIDI KUWAGARAGAZA WENZAKE SIMBA SC….MAMBO YAKE SIO POA AISEE..

admin May 5, 2023 3:33 pm

Mbavu ya kushoto ya Simba SC, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR’ ameongoza kwa kucheza mechi nyingi zaidi kwenye kikosi hicho kwa kucheza dakika 2138 katika msimu huu wa Ligi 2022/23.

Nyota anayemfuatia kikosini hapo ni Aish Manula ambaye amecheza dakika 2026, Henock Inonga (1927), Mzamiru Yassin (1881) na Shomari Kapombe ambaye amecheza dakika 1867.

Kwenye michezo 27 ambayo Simba wamecheza mpaka sasa, Zimbwe amecheza mechi 24 akiwa hajafunga lakini amesaidia (assist) kupatikana kwa mabao 5.

Aishi Manula, yeye amecheza mechi 23 akiwa hajaruhusu goli katika michezo 12 (clean sheet).

Mzamiru amecheza mechi 24, akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana (assist) kwa mengine matano.

Inonga, mlinzi wa kati wa Simba, yeye amecheza mechi 23 akifunga mabao matatu. Kapombe ambaye ni mlinzi wa kulia, amecheza 21 na kufunga magoli mawili

KISA KAULI YA ‘KUFA KIUME’….MCHAMBUZI BONGO AWASHUKIA SIMBA SC….”KILA MWAKA WANAISHIA HAPO HAPO TU”… MBRAZILI SIMBA AANDAA PANGA ZITO…MASTAA HAWA KUPIGWA CHINI…NABI AKABIDHIWA BRUNO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply