Messi to Saudi
Habari za michezo

WAARABU WAPANGA KUMFANYIA KUFRU YA DUNIA MESSI…MSHAHARA WAKE WA RONALDO CHA MTOTO…

admin May 5, 2023 3:20 pm

Serikali ya Saudi Arabia imeandaa ofa kubwa zaidi katika historia ya soka la nchi hiyo ili kumnasa Nahodha na Mshambuliaji wa Mabingwa wa Dunia, Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi.

Matajiri hao wanataka kutengeneza historia mpya kwenye ligi ya Saudia, wakitaka kuwa na miamba miwili ya soka duniani, akiwemo Cristiano Ronaldo anayecheza Al-Nassr FC.

PSG, huenda ikawa bila Messi msimu ujao baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kutofanyika hadi sasa, huku tetesi zikidai PSG ina mpango wa kupunguza mastaa kwenye timu yao.

Kama dili la Messi litatiki basi anaweza kulipwa Pauni milioni 320 kila mwaka, karibu mara mbili ya Pauni milioni 165 anazolipwa Ronaldo.

Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu 2022/23, huku baba yake mzazi Jorge, akiripotiwa kuiarifu klabu hiyo ya Ufaransa kuhusu uamuzi huo mwezi mmoja uliopita.

KUHUSU SAKATA LAO NA FEI TOTO….YANGA WAPEWA NJIA HII NYEPESI YA KUMALIZA KESI KWA USHINDI… NABI :- HAWA WASAUZI MBONA MAPEMA TU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply