BACCA AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI WA YANGA ZANZIBAR
Beki wa kati wa Yanga SC, Bacca, amekiri wazi makosa yake aliyofanya kwenye mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Azam FC. Katika mechi hiyo, Bacca alifanya kosa baada ya kujifunga goli la kichwa na kusababisha yanga kutolewa na kukosa nafasi ya kucheza fainali. Mashabiki wengi walikasirika na kuanza kumkosoa.
Baada ya Yanga kukosa fainali, Bacca alikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka. Hata hivyo, mchezaji huyo hakutoa kauli yoyote hadharani hadi leo alipopata nafasi ya kujibu kwa vitendo uwanjani, Leo Yanga imekutana tena na Azam FC katika mchezo wa NBC Premier League unaochezwa Zanzibar. Tofauti na mechi iliyopita, Bacca alionekana akiwa na hali mpya.
Dakika za mwanzo tu za mchezo, alipokea pasi nzuri ndani ya eneo la hatari na upiga goli la kichwa kali lililotikisa nyavu, akiifungia Yanga bao la kwanza la mchezo, Baada ya kufunga bao hilo, Bacca hakushangilia kwa furaha kubwa. Badala yake, alielekea mbele ya kamera na kuomba msamaha kwa mashabiki wa Yanga.
Afisa habari wa Yanga Ali kamwe pamoja na baadhi ya mashabiki wameonekana kufurahishwa na kitendo cha ibrahim bacca kushinda goli na kuomba msamaha kwa mashabiki wa yanga sc.