Habari za Simba SC
Habari za michezo

KISA SIMBA KUFUNGWA JANA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA ‘KICHAMBO KIPYA MJINI’..

admin May 8, 2023 3:08 pm

Siku moja baada ya Simba SC kuondoshwa kwenye miashindano ya kombe la Shirikisho la Azam, Msemaji wa Yanga  Haji Manara ameibuka na kutupa jiwe la gizani.

Manara ambaye zaidi ya Misimu 5 nyuma alikuwa akifanya kazi Simba  kama Msemaji na Afisa habari, emibuka na kijembe kwenda kwa waajiri wake hao wazamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa sasa nchi imetulia, akimaanisha kuwa mashabiki wa Simba hawana cha kutamba tena,

Itakumbukwa kuwa , Simba SC imetolewa kwenye kombe hilo ambalo lilikuwa ni pekee walilokuwa wakishindania baada ya kupoteza matumaini ya kutwa ubingwa wa ligi kuu.

Simba pia walipoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Afrika baada ya kuondoshwa na Wydad Casablanca ya Morocco kwenye hatua ya Robo fainali.

Kwa kufungwa hapo jana na Azam FC, sasa Simba watamaliza msimu huu bila kushindwa taji lolote lile, kwani mataji yote ya ndani wameshatolewa na mengine hawakuweza kufua dafu.

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara Ameandika….

“Morning Tanzania yangu Morning My People Morning Wananchi Morning Afrikaaaaaaa

Maana ya kilomolomo kwishnehi ndio hii sasa,

Nchi imetuliaaaaaaa, Tuliiiii, na hv ndivyo tunavyotaka Yanga Afrika.

AHMED ALLY:- AZAM FC HAWAJATUFUNGA KWA BAHATI MBAYA…WAMEKUWA KIKWAZO SANA KWETU.. WAKATI MANULA AKIINUA MIKONO MAPEMA…HIVI NDIVYO DIARRA ANAVYOMTIMULIA VUMBI KWA UBORA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply