Habari za Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA KUFUNGWA MAGOLI YA ‘KIZEMBE’ JUZI….ALLY SALIM AIBUKA NA KUJITETEA KWA HILI…

admin May 9, 2023 8:11 pm

Mlinda Lango wa Simba SC Ally Salim amesema ni bahati kwake kupata nafasi ya kuitumikia kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara msimu huu na anatakiwa kuongeza umakini.

Salim amekaa langoni mwa Simba SC katika michezo kadhaa muhimu hivi karibuni kutokana na Mlinda Lango chaguo la Kwanza Aishi Manula kuwa na majeraha na kocha wa timu hiyo, Robert Oliviera ‘Robertinho’ kumtumia yeye badala ya Beno Kakolanya ambaye alikuwa chaguo la Pili.

Salim amekiri ni bahati kupata nafasi hiyo iliyokuwa adimu kwake miaka mingi, ila funzo alilopata ni kuongeza nidhamu kuanzia mazoezi kujiamini na kusikiliza zaidi maelekezo ya kocha.

“Simba ni timu kubwa yenye maono makubwa. Ukifanya vibaya unaumiza mioyo ya watu, ukifanya vizuri unaleta utulivu na amani za mashabiki.”

“Jambo kubwa zaidi nililojifunza kwenye mechi nilizocheza ni kuongeza umakini dakika zote 90, kwani kila timu inakuwa na lengo la kutikisa nyavu ili kupata hitaji lake,” amesema Mlinda Lango huyo kutoka Zanzibar

Ikumbukwe katika michezo ambayo amefanikiwa kudaka kipa huyo ni dhidi ya Ihefu, Young Africans, Namungo (Ligi Kuu Tanzania Bara), Wydad AC (Ligi ya Mabingwa Barani Afrika) na Azam FC (Kombe la Shirikisho ASFC).

MBALI NA HESHIMA KESHO NI VITA KATI YA MAYELE NA RANGA…HUYU MSAUZI NI BALAA SIO KITOTO… MASTAA YANGA WAWALIA KIAPO WASAUZI…MORRISON NDIO KABISAA HATAKI MZAHA YANI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply