Dilunga akiwa Simba SC
Habari za michezo

KUHUSU TIMU GANI ATAICHEZEA MSIMU UJAO…DILUNGA AIKANA SIMBA…AIITA YANGA MEZANI…

admin May 13, 2023 1:21 pm

Kiungo wa zamani wa Simba SC, Hassan Dilunga amesema msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara yupo tayari kucheza timu yoyote ikiwemo Yanga lakini kipaumbele chake cha kwanza ni maslahi.

Dilunga amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuumia wakati akiitumikia Simba SC.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na JKT Tanzania amesema; “Nipo tayari kucheza popote kikubwa maslahi, atakaekuja vizuri na tukaelewana nae ndiko nitakapocheza.”

Kuhusu kurudi Simba SC amesema; “Naendelea kuwasikilizia nafanya nao tu mazoezi kama ambayo ninavyofanya na Mtibwa na timu zingine.”

Hata hivyo Mchezaji huyo ameushukuru uongozi wa Simba SC kwa kumtibu kwa ufasaha kipindi alichokuwa akiumwa.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa Simba wamenipambania kuhakikisha napata tiba sahihi, nimepata nawashukuru nimepona kwa asilimia 100,” amesema Dilunga

RIPOTI YA MBRAZILI…SIMBA KUSAJILI KIKOSI KIZIMA…BAJANA WA AZAM NA KIPA LA VIPERS NDANI… KUHUSU BALEKE KUBAKI TZ…TP MAZEMBE WAZIDI KUIKALIA KOONI SIMBA…TIMU ZA ULAYA ZAWEKA OFA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply