Tetesi za usajili Yanga
Habari za michezo

HII HAPA MASHINE YA KAZI KUTOKA ASEC MIMOSAS INAYOKUJA YANGA…SHABANI DJUMA ATAFUTE PAKWENDA..

admin May 24, 2023 7:02 am

Tetesi zinaeleza kuwa Yanga wanamfuatilia beki wa kulia wa ASEC MIMOSAS ya Ivory Coast, Yao Kouassi Attohoula mwenye umri miaka 26.

Beki huyo anasifika kwa uwezo mkubwa wa kukaba na kupandisha mashambulizi bila kusahau kupiga krosi za maana.

Msimu huu kwenye ligi ya Ivory Coast amefunga mabao 2 na pasi 7 za mabao huku kwenye Shirikisho akipiga pasi 3 za mabao.

Djuma Shabani inaelezwa kocha Nabi ameanza kuingiwa na mashaka juu ya uwezo wake katika siku za hivi karibuni kushindwa kuendana na kasi ya wapinzani jambo ambalo limepekea beki wa kati Dickson Job kupewa upande wa kulia.

Toka kuanza kwa msimu huu, Djuma akuwa kwenye kiwango kizuri hali iliyopelekea aliyekuwa kocha wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera kudai kuwa beki huyo amenenepeana mno.

Djuma alisajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitoka nchini Congo kwenye klabu ya AS Vita ambapo alikuja pamoja na Mayele, Bangala na Moloko.

Msimu wake wa kwanza Yanga ulikuwa wenye mafanikio ambapo alifanikiwa kucheza karibu mechi zote za kimashindano kabla ya kuanza kupata ushindani wa namba msimu huu.

YANGA MPYA HII HAPA…HUKU MAYELE KULE CHIVA…ISHU YA SAIDOO NA SIMBA IKO HIVI… YANGA WATAKA BILIONI 5 KUMUUZA MAYELE…MAMELOD, AL HILAL NA MAZEMBE KUTUMA OFA NONO ZAIDI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply