Habari za Yanga
Habari za michezo

HAYA SASA YANGA WASHINDWE WENYEWE TU…CAF YAWAPANGIA REFA ‘MSWAHILI’ MECHI YA JUMAPILI..

admin May 26, 2023 10:40 am

Refa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean-Jacques Ngmbo Ndala ndiye atakayechezesha Fainali ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Ngmbo Ndala atasaidiwa na Mkongo mwenzake Olovier Kabene Safar na Zakhele Thusi Granville Siwela wa Afrika Kusini watakaokuwa wanakimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja kulia na kushoto.

Mchezo wa marudiano utafuatia Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litatoa orodha nyingine ya waamuzi.

Kufika hatua hii, Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini, wakati USM Alger imeitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

MBRAZILI SIMBA AFANYA KWELI….AKABIDHI ‘FAILI’ KWA MABOSI LENYE MASTAA WA KUTIKISA AFRIKA… YANGA WAMKUNJULIA ROHO FEI TOTO…JINA LAKE KUTAJWA KWENYE FAINAL YA CAF JUMAPILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply