Habari za Simba sc
Habari za michezo

MCHAMBUZI :- MZAMIRU HASTAHILI TUZO MBELE YA AUCHO…APEWE TUZO YAKE BINAFSI..

admin May 28, 2023 1:35 pm

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Justine Kessy, amedai kuwa kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin hakupaswa kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya kiungo bora wa Mwaka.

Justine Kessy amesema hayo baada ya kuibuka mjadala kuhusu kuachwa kwa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho huku akibainisha kuwa kwa maoni yake, Aucho amekuwa bora katika msimu huu ikilinganishwa na Mzamiru.

“Ukitazama kiungo cha Yanga, kwa asilimia kubwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi huwezi kumwacha Khalid Aucho. Amekuwa engine kubwa sana kwenye kiungo cha timu hiyo msimu huu”

“Kwakuwa Mzamiru atakuwa amezidiwa na namba zangu mimi ninazozitazama kwa kiungo iwe mkabaji au mshambuliaji, hakustahili kwenye kuwania tuzo ya kiungo bora. Nadhani alistahili tuzo ya mchezaji aliyeboresha kiwango ‘most improved player’ kama ingekuwepo,” amesema Justine Kessy.

MERIDIANBET WAZIDI KUSOGEZA MAMILIONI DAR…UBUNGO WAFIKIWA KIBINGWA… WAKATI MASHABIKI SIMBA WAKINUNA…KIBADENI AOMBA JEZI YA YANGA AKAFANYE KAZI YAKE MAPEMA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply