Habari za Simba SC
Habari za michezo

MABILIONI YA CAF YAMTIA ‘WAZIMU’ MBRAZILI SIMBA…MABOSI SIMBA MWENDO WA KICHEKO TU…

admin May 28, 2023 1:08 pm

Uongozi wa Simba, umemuhakikishia kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wataweza kumsajili mchezaji yeyote atakayemtaka kuelekea katika msimu ujao kutokana fungu kubwa la fedha wanazotarajia kupewa na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’.

Simba inatarajia kuvuna fedha kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zikiwa ni maandalizi ya Super League lakini pamoja na zile za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, ambazo ni ni Dola 900,000 (zaidi ya Sh 2.1 Bilioni).

Akizungumza nasi, Mkuu wa Idara Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally alisema kwa fedha wanazozipata kutoka CAF ikiwemo Super League na vyanzo vyao vingine vya fedha ikiwemo kwa mwekezaji wao Mohammed Dewji (Mo Dewji) zitawasaidia kumchukua mchezaji yoyote atakayehitajika ndani ya kikosi hicho.

“Tumekuwa na mzigo mkubwa ikiunganisha fedha za mwekezaji wetu, Mohammed Dewji, vyanzo vya Simba pamoja na fedha za Super League hali hiyo tutafanya usajili mkubwa na tunaweza kununua klabu 15 za hapa ndani na hii inamanisha tunapokea mzigo mkubwa.

“Tuko katika mawindo makali tunaangalia watu kadha wa kadha ndani na nje ya Tanzania, Bajana tunamkubalia sana ni kijana ambaye ni mzuri, kocha Robertinho (Roberto Oliveira) akipendekeza basi tutafanya mazungumzo na Azam kupata huduma yake,” alisema Ally.

BAADA YA KUSIKIA FEI TOTO ANACHANGISHA PESA ZA KWENDA CAS…INJINI HERSI AIBUKA NA HILI JIPYA… KUHUSU DILI LA KIBABAGE KUTUA YANGA MSIMU UJAO …ISHU NZIMA KUMBE IKO HIVI AISEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply