Habari za SImba SC
Habari za michezo

M’BAYA WA SIMBA MIKONONI MWA YANGA….MAMBO YAPELEKWA KIMYA KIMYA AISEE..

admin May 29, 2023 2:19 pm

Mwamba aliyepeleka kilio kwa Simba SC, Prince Dube, ameingia mikononi mwa Yanga kwa kuwa kwenye kipengele kimoja cha kuwania tuzo.

Dube aliwatungua Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports likiwa la ushindi, ilikuwa Mei 7, 2023 ubao wa Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliposoma Azam FC 2-1 Simba.

Bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Dube dakika ya 73 na kuwafungashia virago Simba kwenye mashindano hayo.

Katika orodha iliyotolewa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wachezaji watano wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, (ASFC).

Dube na Abdul Suleiman ‘Sopu’ wote wa Azam FC, Bakari Mwamnyeto, Fiston Mayele na Clement Mzize wote kutoka Yanga.

Mastaa wote hao watakutana kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo bingwa mtetezi ni Yanga.

SIKU MOJA BAADA YA YANGA KUFUNGWA …FEI TOTO AIBUKA NA JIPYA HILI TENA…”NATAMANI KURUDI”… SIMBA YAGWA BARUA KWA MASTAA…WAARABU WAONDOKA NA MAYELE DAR…MTZ AINGIZA MIL 200 KWA SAA 2…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply