Habari za Yanga SC
Habari za michezo

BAADA YA KUCHAPWA JUZI…NABI AVUNJA UKIMYA YANGA…AANIKA WALIOFELISHA MIPANGO…

admin May 31, 2023 3:03 pm

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga Nasreddine Nabi ametaja sababu ya kukosa ushindi kwenye mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ambao ulichezwa juzi kwa Mkapa.

Yanga walichapwa mabao 2-1 kutoka kwa USM Alger na kuweka kwenye wakati mgumu wa kuchukua kombe hilo na Nabi amesema hawakupata muda wa kutosha kujiandaa kuelekea katika mchezo huo kama ambavyo ilitakiwa.

Nabi alisema maandalizi hayakuwa bora sana kama ambavyo walitakiwa kuwa nayo kwa sababu walikuwa na muingiliano wa ratiba hapa katikati na ndiyo maana imetokea hiki kilichotokea.

“Maandalizi yetu ni magumu, hatujapata muda wa kutosha, tumetumia muda mwingi kwenye ‘recovery’, tunataka tutoe wito kwa wanaoandaa ratiba tunaliwakilisha taifa, tunaomba siku zijazo lisitokee tena.

“Wachezaji walihitaji muda wa kupumzika na wakati wa kujiandaa. Hakuna namna nyingine, tunakaa na kuona tunachezaje mechi ya marudiano kwa sababu hata hivyo hatuna muda tena wa kutosha,” alisema.

YANGA WAIONYESHA UBABE SIMBA…WATIBUA DILI LA YAHYA MBEGU KIMAFIA MNOO… KISA SIMBA ‘KUFELI’ MSIMU HUU….CHAMA AMTUPIA LAWAMA KOCHA MRAZILI…ADAI YEYE NDIO CHANZO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply