Home Habari za michezo BAADA YA KUONA WATAKUFA VIBAYA LEO…MASAUZI WAOMBA MSAADA KWA SIMBA…

BAADA YA KUONA WATAKUFA VIBAYA LEO…MASAUZI WAOMBA MSAADA KWA SIMBA…

Habari za Michezo

Beki wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Mpho Mvelase ameeleza namna watakavyokuwa na mashabiki wengi katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Yanga SC

Yanga na Marumo zinavaana leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika, ukiwa ni muhimu kwa timu zote mbili.

Akizungumza , beki huyo amesema hawana hofu kwani wanajua Simba wametoka kwenye mashindano ya CAF, hivyo lazima wawe upande wao.

“Simba wote ni mashabiki wetu na watafika kwa wingi kwani sasa hawapo kwenye mashindano ya kimataifa, lazima watatuunga mkono.”

Akizungumzia wachezaji wa Yanga, amesema hakuna anayemfahamu zaidi ya Bernard Morrison kwa sababu aliwahi kucheza naye Orlando Pirates mwaka 2016.

“Morrison ndiye mchezaji pekee ninayefahamu na soka ni mchezo wa makosa kujuana kiufundi hakuwezi kusaidia kuleta matokeo mazuri,” alisema beki huyo.

Mvelase ni mmoja kati ya viungo muhimu wa Marumo na mwenye uzoefu akicheza muda mrefu kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFUNGWA NA SIMBA..KOCHA WA JKT TANZANIA ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA ...