Home Habari za michezo HIVI NDIVYO YANGA INAVYOZIDI KUING’ARISHA TZ KIMATAIFA…LIGI YA BONGO NAYO NG’ARII…

HIVI NDIVYO YANGA INAVYOZIDI KUING’ARISHA TZ KIMATAIFA…LIGI YA BONGO NAYO NG’ARII…

Habari za Yanga

Baada ya Yanga kutinga fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, imeongeza pointi zaidi kwa Tanzania ambapo sasa imepanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 11 msimu uliopita mpaka nafasi ya sita.

Tanzania sasa iko juu ya DR Congo ambayo imeporomoka mpaka nafasi ya saba.

Katika mashindano ya CAF msimu huu Yanga imekusanya alama 20 wakati watani zao Simba ambao walitolewa robo fainali ya ligi ya mabingwa wamekusanya alama 15.

Aidha Yanga imepanda mpaka nafasi ya 18 katika viwango vya ubora wa klabu barani Afrika ikiwa na alama 20.5.

Wananchi wanaweza kupanda hadi nafasi ya 15 kama watatwaa kombe la Shirikisho barani Afrika.

SOMA NA HII  HARUNA MOSHI 'BOBAN' vs CHAMA....NANI AANZE KIKOSI CHA SIMBA ....?