Home Habari za michezo SIMBA WAZIDI KUIKAZIA TP MAZEMBE KWA BALEKE….TAMKO LAO JIPYA HILI HAPA…

SIMBA WAZIDI KUIKAZIA TP MAZEMBE KWA BALEKE….TAMKO LAO JIPYA HILI HAPA…

Habari za Simba SC

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally kupitia kipindi cha #SportsArena ya #WasafiFm amethibitisha kuwa Baleke ni mchezaji halali wa Simba kwa kandarasi ya miaka miwili.

“Baleke ni Mshambuliaji wa Simba amesaini kandarasi ya kuitumikia Simba kwa muda wa miaka miwili, TP Mazembe walipewa pesa yao na ametumikia kandarasi yake miezi minne tu.

“Niwatoe shaka wana Simba ya kwamba Baleke bado yupo sana Simba kwa muda mwingine, mpaka sasa hakuna ofa yoyote kutoka klabu yoyote ikimuulzia Baleke.

“Manula bado anamkataba wa miaka miwili na Simba, bado yupo sana, Mohammed Hussein hana popote pa kwenda duniani zaidi ya Simba,” Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  ORODHA YA NYOTA 10 WA SIMBA WALIOITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA