Home Habari za michezo SIKU ZA MBRAZILI SIMBA SC ZAHESABIKA…..MATAJIRI WA MISRI NA ANGOLA WAMTUMIA OFA...

SIKU ZA MBRAZILI SIMBA SC ZAHESABIKA…..MATAJIRI WA MISRI NA ANGOLA WAMTUMIA OFA NONO..

Habari za Simba SC

Klabu za Al Ittihad ya nchini Misri na Atlético Sport Aviação ya Angola, zimedhamiria kulitikisa Benchi la Ufundi la Simba SC kwa kuanza kummendea Kocha Mkuu wa Klabu hiyo ya Msimbazi Robert Olivieira ‘Robertinho’.

Klabu hizo zinatajwa kumuwania Kocha huyo kutoka nchini Brazil kufuatia mafanikio yake ya muda mfupi tangu alipotua Simba SC ambapo hadi sasa hajapoteza mchezo wa Ligi Kuu, huku akiifikisha Klabu hiyo Robo Fainali na kukosa nafasi finyu ya kutinga Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wydad AC ya Morocco iliyosonga mbele kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Imefahamika kuwa Klabu ya Al Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri imempigia simu kocha huyo ikitaka huduma yake baada ya kuona hesabu zao za kuingia ndani ya klabu tatu za juu kuwa na mashaka.

Al Ittihad sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa Simba SC, Zolan Maki ambaye kabla ya kutua huko alitokea hapa nchini wakiona bado hawajakubali mwendo wa kocha wao huyo raia wa Serbia.

Katika michezo mitano ya mwisho Al Ittihad imeshinda mchezo mmoja na kupoteza mitatu huku wakitoa sare mmoja hatua ambayo imewatisha mabosi wa klabu hiyo wakianza mchakato wa kumsaka kocha mbadala kwa siri.

Kwa upande wa Klabu ya Atlético Sport Aviação ambayo amewahi kuifundisha Mbrazil huyo kwa miaka miwili na kuiacha katika nafasi nzuri inapiga hesabu pia na kumrudisha kocha huyo katika nafasi yake hiyo huku kufuru ikiwa ni fedha za malipo yake.

Hata hivyo Kocha Robertinho amekiri kuwa na ofa kadhaa, huku akisema kwa sasa anataka kukutana na mabosi wa Simba SC kuhakikisha wanamaliza msimu vizuri kwa mashindano ya ndani.

“Ofa hizi ni nyingi kila siku, ni kweli hizo taarifa ninazo lakini kwa sasa nipo hapa Simba SC,” amesema Robertinho

Robertinho alitua Simba SC mwanzoni mwa mwaka huu akitokea kwa Mabingwa wa Soka nchini Uganda Vipers SC ambayo aliifikisha Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuitoa TP Mazembe ya DR Congo.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE :- MATOLA YUKO KWA MASLAHI YA MABOSI WA SIMBA...NI KOSA LA MUDA MREFU SANA...