Klabu ya soka ya Simba SC imepanga kufanya Maboresho Makubwa katika Timu hiyo na eneo kubwa ambalo watafanya Maboresho kuelekea Msimu Ujao ni eneo la Golikipa, ambapo imeelezwa Kocha msaidizi Wa klabu hiyo Juma Mgunda amependekeza jina la Kipa namba Moja Wa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Comoros Mahamoud Mroivili ambaye mkataba wake na Coastal Union unamalizika Mwishoni mwa Msimu Huu.
Tetesi zinasema kwamba kama Simba SC watapata Saini ya Mohamoud atasaini kandarasi ya Miaka Miwili.
Mbali na Simba kuhitaji Saini ya Mohamoud, Timu kadhaa kutoka Nchini Kenya na Afrika kusini zimeonesha nia ya kimhitaji mcomoro huyo.
Mpaka Sasa Mohamoud ana clean sheets 6 kwenye michezo ambayo amekaa langoni akiwa na Coastal Union Msimu Huu.
Timu ambazo amewahi kupita…
Coastal Union FC
Coffee Sport FC ya Ethiopia
Aspl 2000 Club ya Mauritius
Coin-nord Club ya kwao Comoros
Apaches Club ya Comoros
Volcan Club Comoros
Wanamsimbazi vipi Golikipa huyo?
SOMA NA HII PAMOJA NA KUWA WANA KILA KITU...AZAM FC WAIBUKA NA SABABU HIZI ZA KUKOSA UBINGWA ETI....