Fei toto asaini Azam FC
Azam FC

BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM…FEI TOTO AFUNGUKA ISHU YAKE NA RAIS SAMIA…AITAJA YANGA…

admin June 8, 2023 3:52 pm

Aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amewashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho amefanya kazi katika klabu hiyo.

Fei Toto ametoa shukrani hizo mara baada ya kujiunga na Klabu ya Azam akitokea Yanga ambayo ameitumikia tangu mwaka 2018.

“Namshukuru kwa kufikia wakati huu, pia ninamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kufanikisha kumaliza hili jambo hili, ninamuombea kwa Mungu ambariki na amjalie kila la kheri.

“Ninawashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, ninawatakia kila la kheri. Mimi bado naipenda Yanga na mashabiki pia bado nawapenda, asanteni sana,” amesema Fei Toto.

Fei Toto amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia Wauza Ukwaju wa Dar, baada ya kumaliza sakata lake la kimkataba na na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA…INJINIA HERSI ATAJA MFUMO WATAKAOTUMIA… KAMATA MAOKOTO KUPITIA NJIA HII NYEPESI NDANI YA MKEKA WAKO WA CASINO YA MERIDIANBET..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply