Home Habari za michezo WAKATI MJADALA UKIWA NANI ATAPATA TUZO YA UFUNGAJI…MAYELE AKATA MZIZI WA FITINA…

WAKATI MJADALA UKIWA NANI ATAPATA TUZO YA UFUNGAJI…MAYELE AKATA MZIZI WA FITINA…

Habari za Yanga leo

Baada ya msimu wa Ligi kuu soka Tanzania bara 2022/2023 kumalizika huku Wachezaji Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza wa Simba SC wakilingana magoli 17 katika mbio za kuwania tuzo ya Mfungaji bora, Mayele amesema anayestahili Tuzo hiyo ni yeye.

Mayele ameyasema haya wakati akiwa LIVE kwenye Instagram akisherehekea Ubingwa wa Yanga baada ya kuifunga Prisons Jijini Mbeya leo.

“Tushachukua Ubingwa na kiatu tena tunachukua kwa sababu mimi sina goli la penati, wataumia sana leo kwa sababu matumaini yao ilikuwa kiatu”

Mijadala imekuwa mingi mitandaoni na swali kubwa ni nani atapewa tuzo hiyo ukizingatia kwamba kwenye Ligi Kuu Tanzania hakuna kanuni ya moja kwa moja inayoeleza nani atapewa tuzo ikitokea Wachezaji wamelingana magoli japo kuna baadhi ya Mataifa Wachezaji wote hupewa Tuzo (England) huku Mataifa mengine yakimpa Tuzo aliyefunga goli chache za penati.

SOMA NA HII  YANGA INALIPA MISHAHARA MIZURI...YATUMIA BIL 7 KUWALIPA...PACOMEE,AZIZ KI