Home Habari za michezo BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAKARIBIA KUMALIZANA NAYE…KIGOGO YANGA AKABIDHIWA MAKABI..

BAADA YA KUSIKIA SIMBA WANAKARIBIA KUMALIZANA NAYE…KIGOGO YANGA AKABIDHIWA MAKABI..

Tetesi za Usajili Bongo

SASA rasmi uongozi wa Yanga umempa kazi Mtendaji Mkuu (CEO) wa timu hiyo, Mzambia Andrew Ntine ya kuhakikisha anafanikisha usajili wa Mkongomani, Makabi Lilepo kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao.

Yanga inaitaka saini ya mshambuliaji huyo ni baada ya tetesi kuzagaa za straika wao Mkongomani, Fiston Mayele kuwepo katika kubwa ya kuwaniwa na baadhi ya klabu za Afrika Kusini, Iran na Saudi Arabia.

Ikumbukwe Lilepo alikuwa sehemu ya wachezaji wa Al Hilal ya Sudan ambao walifika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Championi Jumamosi, linafahamu mazungumzo yapo katika hatua nzuri ya kuinasa saini mshambuliaji huyo aliyekuwepo katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba katika klabu yake hiyo.

Taarifa ambazo imezipata gazeti hili, Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Ntine ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia usajili wa mshambuliaji ambao umefikia pazuri.

“Rasmi uongozi umeanza mazungumzo rasmi na Lilepo baada ya tetesi nyingi kuzagaa akihusishwa na baadhi ya timu hapa nchini na usajili huo umeachwa kwa Mtendaji Mkuu, Ntine.

“Mazungumzo hayo yanakwenda vizuri kabisa, uzuri ni kwamba amepata ushawishi mkubwa kwa Wakongo wenzake ambao wanaichezea Yanga.

“Uzuri yeye mwenyewe ameonyesha nia kubwa ya kuja kuichezea Yanga kutokana na ofa nzuri aliyopewa pamoja na mafanikio ambayo tumeyapata katika msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili kwa kusema: “Tumepanga kufanya usajili bora utakaoendana na mapendekezo ya kocha wetu, na hakuna mchezaji tutakayemkosa ambaye atahitajika Yanga.”

SOMA NA HII  MORRISON NJIA NYEUPEEE YANGA....NABI AMPITISHA FASTA...ADAI TABIA ZAKE ZA KINIDHAMU SIO ISHU SANA KWAKE...

1 COMMENT

  1. Acha uwongo Lilepo tunae hapa Katanga kwasasa hakuna Kiongozi yeyote wa Yanga waliezungumza zaidi ya wachezaji Mayele na Inongo, mbona mnapenda kutunga