Habari za Michezo
Habari za michezo

KISA KUITWA TIMU YA TAIFA TENA…BANDA AAMUA KULIAMSHA NA HILI…’AJIMIMINIA MINYAMA’…

admin June 21, 2023 4:34 pm

Mlinzi wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Abdi Banda amekiri kufurahishwa kurejea tena kwenye kikosi hicho baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Banda ambaye anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini amesema muda wote yupo tayari kuitumikia timu ya taifa pale atakapohitajika.

“Mimi sio mchezaji wa kusema lazima niitwe timu ya taifa, ninaitwa timu ya taifa kama labda mwalimu ananihitaji kama mwalimu hanihitaji basi sioni ulazima wa kuitwa”, amesema Banda.

Nyota huyo wa Zamani wa Simba anajivunia rekodi za kipekee akiwa na kikosi cha Taifa Stars na anatamani kuendelea kuzilinda rekodi hizo.

“Kitu ambacho ninafurahi ni kwamba sijawahi kupoteza mchezo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hii ni rekodi yangu” amesema Banda.

Abdi banda alijumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger na kutanguliza mguu mmoja kwenye michuano ya mataifa ya Afrika ‘Afcon’ itakayofanyika mwakani nchini Ivory coast.

KUHUSU ISHU YAKE YA KUTUA YANGA …NOVATUS AIBUKA NA HILI…AMTAJA DICKSON JOB…. SIKU CHACHE BAADA YA KUPIGWA CHINI KUTENGENEZA JEZI ZA SIMBA…VUNJA BEI AIBUKA NA KUANIKA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply