Home Habari za michezo WALICHOTETA NABI NA MAYELE LEO AIRPORT HIKI HAPA…YANGA WABAKI ‘MACHO KODO’…

WALICHOTETA NABI NA MAYELE LEO AIRPORT HIKI HAPA…YANGA WABAKI ‘MACHO KODO’…

Habari za Yanga leo

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ametua nchini leo Juni 20 akitokea kwenye majukumu ya timu ya taifa DR Congo.

Mayele alifunga bao katika ushindi wa DR Congo 2-0 ikiifunga Gabon ametua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mke wake na watoto wake.

Mayele akiwa nje ya jengo la abiria la 3 (terminal 3) alikutana na aliyekuwa kocha wake Yanga, Nasreddine Nabi ambaye anaondoka nchini leo.

“Safari njema profesa (Nabi)” ameandika Mayele kwenye ukurasa wake wa Instagram

Wawili hao walipiga picha ya pamoja nje wakati Mayele akiwa na tuzo zake ambazo alishinda msimu wa 2022/23 ikiwemo mchezaji bora Ligi Kuu, mfungaji bora (mabao 17 akifungana na Saido Ntibazonkiza) na bao bora.

Huenda kwa mtazamo wa picha ya mdogo, pengine Nabi alimtaka Mayele amfuate kule anakoenda ambapo inaelezwa kuwa anaienda zake Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Endapo Nabi atakuwa amemweleza hayo Mayele, hii itakuwa na maana ya kuifanya Yanga kuwa mlima mkubwa wa kupanda kwenye kumshawishi kinara huyo wa magoli kwenye klabu yake kubaki.

SOMA NA HII  YANGA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SIMBA KIGOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here