Tetesi za Usajili Ulaya
Habari za michezo

TETESI ZA USAJILI ULAYA:- BARCA WAMALIZANA NA INIGO…..

Staff Desk July 5, 2023 5:24 pm

MABINGWA wa Hispania klabu ya Barcelona ‘La Blaugrana’ imethibitisha kwamba Inigo Martinez atajiunga na timu hiyo kwa uhamisho huru akitokea Athletic Club.

Kwa muda mrefu La Blaugrana imekuwa ikihusishwa na beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 ambaye amecheza mechi 357 za La Liga akiwa Athletic na wapinzani wa eneo la Basque Real Sociedad.

 

Tovuti ya michezo 90min imesema Martinez amekubali kwenda kukipiga Barcelona na wakati wowote atasaini mkataba wa miaka miwili.

“Taarifa kutoka klabu ya Barcelona imesema : Makubaliano yamefikiwa kati ya FC Barcelona na Inigo Martinez kwa ajili ya mchezaji huyu kujiunga na klabu yetu baada ya mkataba wake na Athletic Club kumalizika.”

Martinez atakuwa mchezaji wa pili kusajliwa Barcelona katika dirisha hili la majira ya joto baada ya Ilkay Gundogan kumwaga wino akitokea Manchester City.

KUMEKUCHA….SIMBA YAINGILIA USAJILI YANGA…JEZI NO 6 ATUMIWA MKATABA…MAYELE AKESHA NA MABOSI.. SIMBA SC IMEPANIA KURUDISHA UFALME WAKE BAADA YA KUKOSA MATAJI…. LEO KLABU YA SIMBA IMEMTANGAZA MCHEZAJI WAKE HUYU MPYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply