Habari za michezo
MWANASHERIA WA YANGA ALAMBA DILI FIFA,… YANGA WATIA NENO
Staff Desk
July 9, 2023
6:31 am
Mkurugenzi wa Sheria wa Young Africans SC, Wakili Simon Patrick amechaguliwa na Baraza Kuu la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuwa kwenye jopo la Wanasheria watakaolisaidia Shirikisho hilo kwenye masuala mbalimbali ya kisheria kwa wachezaji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Young Africans SC, imeeleza kuwa Wakili Simon ni Mtanzania pekee kwenye jopo la Wanasheria 21 kutoka sehemu mbalimbali duniani waliochaguliwa na Shirikisho hilo (FIFA) na atahudumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.