Habari za Michezo
Habari za michezo

BAADA YA KIMYA KIREFU…KABWILI AFUNGUKA KUVUTIWA NA DIARRA…AANIKA SIRI HII YA ‘NDANI ZAIDI’…

admin July 14, 2023 8:35 pm

Mlinda lango wa zamani wa Yanga na Rayon Sports ya Rwanda, Ramadhan Kabwili amesema katika makuzi yake ya soka amewahi kufanya mazoezi na magolikipa wote wakubwa na wazuri nchini na ndicho kinachomfanya leo hii anakua bora sana.

Kabwili amesema anavutiwa zaidi na mlinda lango wa klabu ya Yanga Djigui Diarra namna ambavyo anacheza akiwa langoni na anawafundisha makipa wetu kucheza kisasa zaidi.

“Nimepata nafasi ya kufanya mazoezi na magolikipa wengi wazuri na wakogwe Tanzania isipokua Mwameja, kuna vitu vizuri nimenipata kwao”.

Itakumbukwa kuwa Kabwili aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga na Taifa Satrs alijiunga na Rayon Sports mara baada ya Yanga kutangaza kuthitisha mkataba wake kwa kile kilichoelezwa kuwa tabia zake za nnje ya uwanja hazikuwa na picha nzuri kwa klabu.

Mwishoni mwa msimu wa 2021, mitandaoni kulivuja video isiyo ya maadili ikimuonyesha kijana anayedhaniwa kuwa ni Kabwili akiwa katika hali tata inayotia kinyaa kwa mila na desturi za kiafrika.

Hata hivyo, si yeye mwenyewe Kabwili au Yanga waliodiriki kukiri hadharani kuwa video ile sawa na mahisio ya watu.

Kabwili alipata kutamba na Yanga kwa misimu kadhaa nyuma hata kufikia hatua ya kuaminiwa kusimama mlangoni kwenye mechi ngumu ya watani wa jadi dhidi ya Simba.

WAKATI SIMBA WAKIPANGA KUMUAGA MKUDE….MANARA KAIBUKA NA HILI JIPYA…AMETAJA MO DEWJI TENA… BARBARA AZIDI KUKINUKISHA SIMBA….AACHIA ‘DONGO’ LINGINE TENA …

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply