Habari za Simba
Habari za michezo

BARBARA AZIDI KUKINUKISHA SIMBA….AACHIA ‘DONGO’ LINGINE TENA …

admin July 14, 2023 8:41 pm

Siku maoja baada ya Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji kupost ujumbe ambao umezua sintofahamu kwa Mashabiki na wananchama wa Klabu ya Simba SC akidai kuchoka kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa Transformation ndani ya Klabu ya Simba kwa miaka sita.

Juzi Julai 12, aliekuwa CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez ametweet ujumbe ambao umeacha maswali kwa walio wengi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Barbara ameandika;

“Hauwezi kudhulumu haki za watu halafu ukataka amani na mafanikio.”

AKAJA NA HILI TENA

Mapema hii leo Julai 14, 2023, Barbara ameweka ujumbe mpya uliosomeka hivi:

“Ulevi wa madaraka haujawahi kuwa na mwisho mwema.”

Kama kawaida ujumbe huo umezua mjadala na watu kuhoji ni kitu gani kilichopo nyuma ya jumbe hizo zinazoonekana kama kuna watu anawalenga.

Kabla ya ujumbe huo, Barbara aliandika jumbe nyingine tata ambazo pia ziliibua mjadala wa kutosha.

“Usilipize ubaya kwa ubaya, lakini usiwe mnyonge kudai haki zako!”

“Hauwezi kudhulumu haki za watu halafu ukataka amani na mafanikio.”

BAADA YA KIMYA KIREFU…KABWILI AFUNGUKA KUVUTIWA NA DIARRA…AANIKA SIRI HII YA ‘NDANI ZAIDI’… PAMOJA NA KUTUA ZAKE YANGA…MKUDE AIKATAA JEZI NO 6….MABOSI WAMLAZIMISHIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply