Home Habari za michezo HII IMEENDAAAH…..MIQUISSONE ‘IN’…..BANDA ‘OUT’….ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE…

HII IMEENDAAAH…..MIQUISSONE ‘IN’…..BANDA ‘OUT’….ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE…

Tetesi za Usajili Simba

MASHABIKI wa Simba wanaendelea kutambia usajili uliofanywa na mabosi wao hadi sasa, huku utamu zaidi ni taarifa za winga Peter Banda kukubali kumpisha Luis Miquissone anayejiandaa kutua kambi ya timu hiyo iliyopo Uturuki katikati ya wiki hii kurejesha burudani Msimbazi.

Banda ndiye aliyekuwa mrithi wa Luis mara alipouzwa Al Ahly ya Misri na kupewa jezi namba 11 aliyokuwa akiitumia winga huyo kutoka Msumbiji ambaye Simba inamrejesha klabuniĀ  baada ya kumalizana na Wamisri, ingawa alishindwa kuonyesha makali na kuwa majerehu kila mara.

Habari za ndani ya Simba zinasema kuwa, Banda aliyekuwa akigoma kutolewa kwa mkopo akitaka kuvunjiwa mkataba wa mwaka mmoja uliosalia kikosini ili asepe zake na kufanya mabosi wa klabu hiyo kuumiza kichwa kabla ya kupata muafaka na sasa nyota huyo wa Malawi anaondoka Msimbazi.

Sio Banda tu, bali hata winga mwingine kutoka Senegal, Pape Ousmane Sakho naye dili lake la kutaka kuuzwa barani Ulaya limekaa vyema na kutoa nafasi kwa Simba kuyaingiza majembe mawili ya kuhitimisha usajili wa wachezaji wa kigeni kwani kwa sasa tayari ina wachezaji 12.

Wakati Banda anampisha Luis ili kwenda na hesabu ya kanuni ya usajili wa nyota wa kigeni iliyopo Ligi Kuu Bara, kwa upande wa Sakho mara dili lake likitiki itatoa nafasi ya kuingizwa kwa kipa mpya ambapo awali ilielezwa angeletwa Mbrazili Caique Luis da Santos ili kumsaidia Aishi Manula aliye majeruhi kwa sasa, kabla ya dili hilo kusitishwa ili kusikiliziwa kwanza.

Ipo hivi. Simba inapambana kukamilisha dili la Luis na kipa mpya, tayari kikosi ilikuwa na nyota 12 wa kigeni kwa mujibu wa sheria ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lakini kuibuka kwa ofa za Banda na Sakho imewapa nguvu Simba kumalizana na Al Ahly ili kumrejesha Luis.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa, wamepokea ofa ya Banda na wapo tayari kumruhusu kuondoka na wamefanya mazungumzo na Banda ya kumtoa kwa mkopo au kumalizana naye jumla ili waweze kusajili wachezaji wapya wawili wa kigeni wa mwisho.

“Simba imeridhia kumalizana na mawinga hao wawili ili kupisha usajili ambao tunaamini utakuwa na chachu kubwa ya ushindani kutokana na wachezaji wanaotarajia kuingia wanauzoefu mkubwa na mmoja tayari alishafanya mambo makubwa kabla hatujamuuza,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kuhusu Banda hadi sasa sijajua kama atatoka kwa mkopo au anaachwa jumla, lakini taarifa zilizopo msimu ujao hatakuwa mchezaji wa Simba.”

Kwa upande mwingine rafiki wa karibu wa Banda amesema kuwa mchezaji huyo tayari keshaambiwa juu ya dili hilo naye ameridhia kuondoka kutokana na mazungumzo waliyoyafanya japo hakutaka kuweka wazi ni kuvunja mkataba au kuuzwa.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba winga huyo anaondoka suala la wapi anaenda sina majibu zaidi, lakini ameshaniambia kuwa muda wowote ataondoka.”

SOMA NA HII  SIMBA SC YAANIKA MIPANGAO YAKE HII WAZI 2023/24