Habari za michezo

YANGA WATAMBA KUSHUSHA NYOTA MWINGINE HATARI TUPU

Staff Desk July 19, 2023 8:41 pm

RAIS wa Klabu ya Yanga Hersi Said amesema timu hiyo inatarajia kumtangaza mchezaji mwingine mpya kwenye kikosi hicho ili kuongeza nguvu kuelekea msimu ujao.

Mhandisi Hersi Said ameiambia Spotileo Julai 19,2023 kuwa mara baada ya kumtambulisha mchezaji Mahlatsi Makudubela maarufu skudo leo watamtambulisha mchezaji mwingine wa daraja la juu.

“Jana tumemtambulisha mchezaji atakae vaa jezi namba sita, tumeandika historia ya mchezaji raia wa Afrika Kusini kucheza kwenye ligi yetu, na leo usiku tunashusha mchezaji mwingine ambaye alikuwa mchezaji bora kwenye ligi anayotoka”amesema Hersi Said.

Katika hatua nyingine Mhandisi Hersi amesema kwasasa wanajipanga na kilele cha siku ya Mwananchi Julai 22 katika dimba la mkapa ambapo wachezaji wote watakaosajiliwa watakuwepo kwenye tamasha hilo.

YANGA YABAKISHA SIKU NNE KUWASHANGAZA MASHABIKI NA WADAU KOCHA WA YANGA GAMONDI ANENA NA MASHABIKI, ASEMA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply