Yanga SC na Simba SC
Habari za michezo

HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA,YANGA, MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA JULAI 25

Staff Desk July 23, 2023 9:33 pm

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetangaza kufanyika kwa droo ya hatua ya awali kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, Julai 25, jijini Cairo, Misri kuanzia saa 9:00, saa za Afrika Mashariki.

Klabu 54 kutoka mataifa 42 wanachama wa CAF zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, huku klabu 52 kutoka mataifa 41 zikishiriki Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Droo kwa upande wa Ligi ya Mabingwa itahusisha timu 54, huku mbili kutoka Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo ambazo ni Simba SC na Yanga na moja kutoka Zanzibar ambayo ni KMKM.

Kombe la Shikisho linashirikisha timu 52 huku Tanzania Bara itawakilishwa na Azam FC na Singida fountain Gate FC na kwa Zanzibar itawakilishwa na JKU SC

Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika, bingwa msimu uliopita ni Al Ahly ya Misri huku kwenye Shirikisho akiwa ni USM Alger ya Algeria.

YANGA KILA KITU NI FRESH, BADO WENYE NCHI KIPA MBRAZIL ATUA SIMBA, KAIZER YATUA ZANZIBAR DKT MWINYI AIPA BARAKA, HERSI AMKABIDHI JEZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply