simba
Habari za michezo

ROBERTINHO AFUNGUKA HALI YA WACHEZAJI WA SIMBA HUKO UTURUKI SIO POA…….ISHU IKO HIVI

Staff Desk July 31, 2023 1:42 pm

ROBERTO Oliveira ‘Robertinho’, Kocha Mkuu wa Simba, amesema mastaa wake wote walio kambini Uturuki, wamezidi kuimarika kutokana na maandalizi wanayoendelea kuyafanya.

Mbrazili huyo ameanza kuwanoa mastaa waliokuwa katika kikosi hicho ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Kibu Denis na John Bocco.

Mbali na hao, wapo mastaa wapya ambao ni Luis Miquissone, David Kameta, Willy Onana, Che Malone Fondoh na Idd Chilunda.

Julai 27, 2023, Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Turan FC, asubuhi ilipata ushindi wa mabao 2-0 na jioni ilitunguliwa bao 1-0.

Kocha huyo amesema: “Kwa namna ambavyo wachezaji wanajituma kwenye mechi pamoja na mazoezi ninafurahishwa na uwezo wao, taratibu wanazidi kuelewa.

“Ambacho tunaangalia ni kuona namna gani tunakuwa imara kwenye upande wa mazoezi pamoja na utimamu wa kufanya kazi kwa umakini, hivyo ninawapongeza wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi.

“Ushirikiano uliopo ni mkubwa kwa kila mmoja, bado kazi inaendelea na tutazidi kuwa imara kutokana na maandalizi ambayo tunafanya.”

USHINDANI WA MASTAA HAPO SIMBA SIO POA, MATOLA AMUIBIA SIRI MIQUISSONE SIRI IMEFUJA SABABU ZA SIMBA KUMTEMA KIPA WAO MBAZILI…. TATIZO LIMEANZIA HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply