Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MZIKI WA MASTAA WAPYA ….PHIRI KAGUNA WEEEH..KISHA AKASEMA HAYA…

BAADA YA KUONA MZIKI WA MASTAA WAPYA ….PHIRI KAGUNA WEEEH..KISHA AKASEMA HAYA…

Habari za Simba

USAJILI mzito ambao unaendelea kufanywa na mabosi wa Simba umemuibua staa wa timu hiyo Mzambia, Moses Phiri ambaye ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao.

Simba wanafanya vurugu kubwa kwenye dirisha la usajili msimu huu ambapo mpaka sasa wametoa mkono wa kwaheri ‘Thank You’ kwa mastaa na watendaji wao tisa, huku wakiwa wametambulisha wachezaji watatu wapya ambao ni Wacameroon, Willy Onana, Che Malone Fondoh na Muivorycoast Aubin Kramo ambao wanacheza katika nafasi za ulinzi na ushambuliaji.

Phiri ni miongoni mwa mastaa ambao walikuwa na msimu mzuri ndani ya Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akifanikiwa kufunga mabao 10 kabla ya baadae kupata changamoto ya majeraha.

Kikosi hicho mara baada ya kukamilisha utambulisho wa mastaa wapya, watakaokuwa chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kinatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kwenda kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Phiri alisema: “Kila mmoja ana shauku ya kuanza msimu mpya na kupambana kwa ajili ya kuisaidia timu kushinda mataji, tunajua msimu ujao utakuwa mgumu kutokana na kuongezeka kwa ushindani kutokana na ubora wa kila timu, lakini naamini katika ubora wa wachezaji waliopo na wale wapya tutafanya vizuri.”

SOMA NA HII  PAMOJA NA LIVERPOOL KUUKOSA UBINGWA WA EPL DHIDI YA MAN CITY MSIMU HUU ...KLOPP AMBWAGA GUARDIOLA KWA UBORA...