Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI AWAGOMEA MABOSI WA YANGA, MECHI DHIDI YA AS VITA, SASA YANGA KUKIPIGA NA TIMU HII

Staff Desk August 3, 2023 6:57 pm

Kama kuna kitu ambacho Gamondi amewashtua mabosi wake ni uamuzi wake wa kugomea mechi ambayo mabosi wake walitaka timu hiyo ikipige dhidi ya AS Vita ya DR Congo Jumapili, lakini akawaambia hakuna mchezo huo, labda upigwe Avic na hakuna shabiki kuingia.

Vita wako hapa nchini lakini Gamondi amegomea wao kucheza Chamazi na Yanga. Gamondi amewaambia mabosi wa Yanga kwamba atafutiwe mechi nyingine kwa timu ya ndani kisha wakipige kambini na sio Chamazi kwa kuwa atakuwa amekwenda kuuza silaha wakati Ngao ya Jamii ni wiki ijayo.

Tayari mabosi wa Yanga wameshachukua maelekezo hayo ambapo soka la bongo Inafahamu huenda JKU wakashuka mjini kutoka Unguja Zanzibar kuja kujipima na mabingwa hao, na Jumapili hakutakuwa na mechi kama ilivyotangazwa awali.

YANGA WAJA NA JIPYA KUHUSU MSIMU WA 2022/23 ISHU IKO HIVI SIMBA HII UNATOKAJE KWA MFANO,….. GAMONDI AJIONEA BATO LA MABEKI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply