Habari za Simba leo
Habari za michezo

BAADA YA KUANZA KUKIWASHA KWENYE SIMBA DAY….ONANA AJA NA TAMBO ZA ‘KIMWAKINYO’….

admin August 8, 2023 7:19 pm

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Mcameroon, Willy Essomba Onana, ameanza tambo jeuri kwa kuwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba, moja ya mipango yake ndani ya timu hiyo ni kuona anafanikiwa kufunga mabao katika kila mchezo.

Onana ametoa kauli hiyo kufuatia kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia, ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa juzi Jumapili (Septemba 06) kwenye Tamasha la Simba Day, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Onana amesema amefurahi kuwa miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kufunga katika mchezo huo, huku akisisitiza kwamba amejipanga kufunga sana ili kufikia malengo ya timu hiyo katika michuano ya kimataifa.

“Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa mmoja kati ya wachezaji waliofunga bao katika mchezo mkubwa mbele ya mashabiki wengi ambao wamejitokeza kutupa sapoti, hili ni jambo kubwa kwangu, lakini bado kuna kazi kubwa iliyopo mbele yetu.

“Nadhani hapa ni mwanzo kwa sababu nataka kuona nafunga sana katika kila mchezo ambao nitaweza kucheza kwa lengo la kusaidia timu katika mashindano ambayo tunaenda kushiriki, kikubwa mashabiki kuendelea kutuombea na kutupa sapoti ya kutosha kwa kufika katika mechi zetu.” amesema Onana.

HUU HAPA MKWANJA WALIOLIPA SIMBA KUMPATA KIPA WA KMC HUSSEIN ABEL… USIFIKIRI UKO MWENYEWE….HUYU HAPA STAA MWINGINE MKUBWA ANAYEKULA MAISHA KWA KUBET TU..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply