Habari za Yanga
Habari za michezo

MENEJA WA YANGA NAE AJA NA HILI KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA

Staff Desk August 11, 2023 4:04 pm

Meneja wa Klabu ya Yanga, Walter Harson jana amezungumzia hali ya kikosi chao kuelekea maandalizi ya mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii utakaopigwa siku ya Jumapili, Agosti 13, 2023 katika Dimba la CCM Mkwakwani dhidi ya watani zao Simba Sc.

Yanga imetinga fainali baada ya kuifunga Azam FC bao 2-0 juzi Agosti 9, huku Simba wao wakitinga fainali baada ya kuiondosha Singida Fountain Gate kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kumalizika kwa dakika 90 bila kufungana.

“Kwanza kabisa ni kocha kuweza kuwapongeza wachezaji kwa jinsi ambavyo waliweza kujitoa kwenye mchezo wa jana (juzi). Sasa hivi mazoezi yanaendelea lakini pia recovery kwa wale ambao wameweza kucheza mchezo wa jana.

“Kwahiyo kuna makundi mawili ambayo yanafanya mazoezi tofauti, baada ya hapo tutaendelea siku ya kesho (leo) na kesho (leo) kutwa kabla ya mchezo wa Fainali. Kwahiyo kila kitu kipo sawa hadi sasa hivi,” amesema Walter.

MOLOKO KURUKA NA SIMBA SASA AUGUST 13 ROBERTINHO ALALAMIKA HUKU AKIWAPA ONYO YANGA!!! NOMA KWELI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply