Burudani

MAYELE AIKATAA YANGA HADHARANI MBELE YA MASHABIKI, ASEMA YEYE SIO SHABIKI WA YANGA, TIMU YAKE HII HAPA

Staff Desk August 12, 2023 9:19 am

Mshambuliaji wa zamani wa AS Vita Club ya Congo na Yanga SC, Fiston Kalala Mayele ambae kwa sasa nakipiga kwenye Klabu ya Pyramids FC ya Misri amekataa kuwa yeye si shabiki wa Yanga bali ni Shabiki wa As Vita.

Mayele ametoa majibu hayo baada ya shabiki wa Yanga @akili5000 kumchokonoa kwenye comment katika picha aliyospost mchezaji huyo kwa kuandika; “Shabiki mkubwa wa Yanga anaecheza Pyramid.”

Baada ya comment hiyo Mayele alijibu kwa kuandika; “Mimi ni Shabiki wa As Vita bana.”

Ikumbukwe kuwa Mayele alijiunga na Yanga msimu wa 2021/22 ambapo ameitumikia timu hiyo kwa miaka miwili mpaka mwishoni wa msimu ulipomalizika akiwa ameisaidia kushinda mataji sita ya ndani kwa miaka miwili, kufika fainali ya CAFCC na yeye mwenyewe kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC na mfungaji bora wa michuano ya CAFCC.

Yanga walihitaji zaidi kumbakisha Mkongomani huyo lakini Waarabu walimwaga mkwanja wa kutosha ambao ulimshawishi kuachana na mabosi zake hao wa Jangwani na kutimkia Misri hivi karibuni.

MTATOKEA WAPI! CHAMA KUKIWASHA NA ONANA PALE KATI, YAO, MAXI KUTEKA SHOO TANGA SIMBA WALIAMSHA DUDE WATOA KAULI NZITO HUKO SUPER LEAGUE, SIO AL AHLY WA MAMELODI KAZI IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply