Habari za Michezo
Habari za michezo

WADAU WAITABIRIA YANGA KUNYAKUA NGAO YA JAMII ISHU IKO HIVI

Staff Desk August 12, 2023 12:11 pm

Baadhi ya wachambuzi wa soka na wadau wa kabumbu nchini wanaipa Young Africans Sports zaidi ya asilimia 50 kushinda taji la Ngao ya Jamii mbele ya mtani wake Simba SC huku wakitoa sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu ikiwa ni pamoja na muunganiko mzuri uliyopo ndani ya kikosi cha Yanga, wakati Simba wakionekana bado wanajitafuta ili kuupata muunganiko.

Pili matokeo kwenye mechi zao za hivi karibuni ikiwemo zile za utambulisho wa wachezaji na hizi mbili za mwisho za Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

Yanga SC wameonekana imara zaidi hata kupelekea kushinda goli 2-0 dhidi ya Azam FC, wakati Simba SC akilazimishwa sare tasa ya 0-0 mbele ya Singida Fountain Gate FC mpaka kupelekea kupigwa mikwaju ya penati.

Kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram ya timu hizi Yanga SC wapo ‘serious‘ na mazoezi wakati Simba SC bado wana Furaha ya Kutinga Fainali kwa kumfunga Singida kwa mikwaju ya penati (4-2).

SIMBA WALIAMSHA DUDE WATOA KAULI NZITO HUKO SUPER LEAGUE, SIO AL AHLY WA MAMELODI KAZI IPO HIVI WAKATI WOWOTE SASA SIMBA WANAMTAMBULISHA KIPA HUYU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply