Habari za Yanga leo
Habari za michezo

MAKOCHA SIMBA, YANGA, AZAM WAKOSA SIFA, TFF YACHUKUA MAAMUZI MAGUMU

Staff Desk August 15, 2023 6:37 pm

Kocha Mkuu wa Azam FC Youssouf Dabo ameondolewa kwenye orodha ya Makocha watakaokaa kwenye Mabenchi ya Ufundi wakati wa Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24, ambayo rasmi imeenza leo Agosti 15.

Dabo ambaye alianza kazi rasmi Azam FC wakati wa maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’ ameenguliwa kwenye orodha hiyo, kufuatia kukosa vigezo vya taaluma vinavyotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ na lile la Barani Afrika ‘CAF’.

Kocha mwingine aliyeenguliwa kwenye orodha hiyo ni Kocha Msaidizi wa Simba SC Ouannane Sallami pamoja na Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana. Naye Kocha Msaidizi wa Young Africans Moussa Ndaw amepitiwa na panga hilo, sambamba na Kocha Mkuu wa Coastal Union Mwinyi Zahera.

MUAMUZI WA SIMBA vs YANGA AFUNGUKA UTATA KUHUSU PENATI ZA SALIM ALLY, ISHU IKO HIVI YANGA WAPIGA MOYO KONDE KUHUSU NGAO YA JAMII, WAELEKEZA NGUVU HUKU, UONGOZI WAFUNGUKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply