simba
Habari za michezo

SIMBA ATAMBA UGENINI, AWANYOOSHA WALIMA MIWA MANUNGU

Staff Desk August 17, 2023 7:14 pm

IKIWA Uwanja wa Manungu, Morogoro katika safu za milima ya Uluguru, Mtibwa Sugar imeyeyusha pointi tatu.

Ubao umesoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba ukiwa ni mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Katika mchezo wa Agosti 17 Uwanja wa Manungu, Mtibwa Sugar walikuwa imara kwenye mashambulizi ya kushtukiza pamoja na kujilinda kwa tahadhari huku wakikosa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Mabao ya Simba yamefungwa na Jean Baleke dakika ya tano, Willy Onana dakika ya 9, Fabrice Ngoma dakika ya 44 na Clatous Chama dakika ya 80.

Mwamba aliyewatungua Simba dakika 45 za mwanzo ni Matheo Anthony ilikuwa dakika ya 20 na 22 kwa Mtibwa Sugar amemtungua Ally Salim mabao yote mawili.

ZINGATIA ALAMA HIZI KISHA WEKA DAU LAKO KWENYE SLOT YA EMPIRE GOLD USHINDE KIBUNDA… GAMONDI AZIPELEKA SILAHA MAFICHONI,… SIMBA WAPIGA HESABU ZA BILIONI 29

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply