Habari za Yanga
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA MORRISON KUISHITAKI YANGA FIFA…UKWELI WOTE A-Z HUU HAPA….

admin August 20, 2023 4:15 pm

Inaelezwa kuwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison huenda akaishtaki Young Africans kwenye Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu kabisa na Kiungo huyo aliyeitumikia Young Africans na Simba SC kwa nyakati tofauti zimeeleza kuwa Morrison anaweza kwenda tena FIFA kuwashtaki Yanga kama fedha hizo na kama ikiendelea kuwa hivi ilivyo sasa, hatakuwa na jambo lingine zaidi ya kuomba msaada FIFA.

Mtoa taarifa huyo amesena, ameambiwa na Morrison kuwa amewapa Young Africans muda wa kuhakikisha kuwa analipwa.

“Morrison amesema kuwa amewapa muda Young Africans na wakishindwa kumpa stahiki zake atawashtaki FIFA, ingawa hajasema kuwa ni kiasi gani na fedha za nini.

“Kubwa amesema kuwa kama huo muda ambao ametoa hatolipwa ndiyo atakwenda FIFA ili aweze kupewa haki yake,” alisema mtu huyo.

Alipotafutwa Morrison mwenyewe ili kuweza kujibia taarifa hizo ilikuwa ngumu kumpata, ingawa mtu wake wa karibu alisema kuwa yupo Morocco kwenye klabu ya FAR Rabbat inayonolewa na Nasreedin Nabi akimalizia taratibu za kujiunga na timu hiyo.

GAMONDI AWEKA WAZI MPANGO HUU KIMATAIFA YANGA ITUMIE SLOT YA FOXPOT KUKUSANYA MTONYO KWA KILA DAU UNALOWEKA KWENYE MKEKA WAKO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply