Habari za Yanga
Habari za michezo

GAMONDI AWAWEKEA MKAKATI WA HATARI KMC LEO

Staff Desk August 23, 2023 2:07 pm

LEO Jumatano Agosti 23, 2023 Yanga ikitarajiwa kuvaana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa, atahakikisha anapanga kikosi cha maangamizi.

Yanga itapambana na KMC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya ASAS Djibouti.
Gamondi amesema: “Bado ninaendelea kuandaa kikosi changu, ila kwa kuwa naenda kucheza mchezo wa kwanza wa ligi na timu bora ya KMC, nitahakikisha naenda kushinda mapema zaidi ili kujitengenezea nafasi bora kwenye ligi katika mchezo wetu wa kwanza,” alisema.

Yanga ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wanaanza karata ya kutetea taji lao baada ya kushindwa kufanya hivyo awali kutokana na kuwa na majukumu ya mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS Djibouti.

ROBERTINHO AANZA KUTOA LUGHA TATA,,,,, ISHU IKO HIVI PHIRI ATAMBA, ATANGAZA HALI YA HATARI KWA AZAM, YANGA……ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply