Habari za michezo
MCHAMBUZI :- ZOUZOUA WA YANGA SI MCHEZAJI WA KUTEGEMEA…
admin
August 25, 2023
7:24 pm
Mchambuzi maarufu wa soka nchini kupitia channel ya runinga ya TV3, Alex Ngereza amesema kuwa licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa juzi dhidi ya KMC, kiungo mpya wa Yanga Sc, PacΓ΄me Zouzoua si mchezaji wa kutegemea.
Zouzoua ambaye amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast ameonyesha kiwango bora katika mechi alizocheza hasa yaΒ juzi huku akiisaidia timu yake kushinda bao 5-0 na yeye akiweka msumari wa mwisho.
“PacΓ΄me Zouzoua alianza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza lakiniΒ ndio siku ya kutuonyesha uwezo wake. Ingawa kwangu mimi bado sioni kama anaweza kuwa mchezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Yanga,” amesema Alex Ngereza.
Yanga sasa inahesabu alama tatu na bao 5 ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu baada ya kucheza mchezo mmoja tu ambao unaonyesha Yanga wamedhamiria kutetea taji lao kama ambavyo wamekuwa wakijinasibu.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.