Home Habari za michezo KUHUSU SIMBA KUTUMIA BILIONI 3 KWA KIPA MPYA….?, UKWELI WOTE HUU HAPA…

KUHUSU SIMBA KUTUMIA BILIONI 3 KWA KIPA MPYA….?, UKWELI WOTE HUU HAPA…

Habari za Simba leo

KLABU ya Simba, imefanikiwa kumsajili kipa raia wa Morocco, Ayoub Lakred, akitokea FAR Rabat ambapo anaenda kuungana na Ally Salim, Hussein Abel na Aishi Manula ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Transfermarkt unaojihusisha na masuala ya takwimu na uhamisho wa wachezaji, thamani ya kipa huyo kwa sasa ni euro 1,200,000, sawa na Shilingi 3,281,436,000 (bilioni 3.3) za Kitanzania, hivyo Simba imefanikiwa kutoa kitita hicho kukamilisha usajili wake.

Kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuanzia Agosti 11, 2023 na unatarajiwa kufikia tamati Juni 30, 2025.

Hivi karibuni Rais wa Heshima wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, alisema: “Nimetoa karibia bilioni 3 kufanikisha huu usajili, isitokee kwamba mtu aseme ‘Mo hajatoa hela’ tuepuke na wapotoshaji.”

Mo aliongeza kwamba: “Ali (Ally Salim) ni mzuri na Aishi ni Tanzania 1, hata hivyo ikiwa tunataka kushindana kwenye Ligi ya Mabingwa, Simba inahitaji kipa mwingine bora.”

Ujio wa Lakred ndani ya Simba, ni baada ya klabu hiyo kuachana na Mbrazili, Jefferson Luis ambaye siku chache tangu kusajiliwa kwake, alipata majeraha wakati timu ikiwa kambini Uturuki.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA SIMBA WANAKUSANYA MAOKOTO KIMYA KIMYA