Habari za Michezo
Habari za michezo

HUYU HAPA ALIYEMFUNIKA SAMATTA NDANI YA PAOK….TOKA ASAJILIWE HAJAFURUKUTA…

admin September 1, 2023 7:42 pm

Timu ya Mbwana Samatta, PAOK Thessaloniki imeanza kibabe msimu huu ambapo haijapoteza mechi zote sita za mashindano tofauti ilizocheza hadi sasa, lakini nahodha huyo wa Taifa Stars bado hajapata muda mwingi wa kucheza chini ya kocha Razvan Lucescu, raia wa Romania.

Katika mechi hizo ambazo PAOK imeshinda nne na kutoka sare mbili, Samatta amecheza michezo mitano, huku minne akitokea benchi na mmoja akianza kikosini, lakini imeonekana mshambuliaji raia wa Hispania, Brandon Thomas ndiye amekuwa kikwazo kwa nyota huyo kupata nafasi ya kucheza.

Brandon (28) aliyejiunga na PAOK mwaka jana akitokea Malaga ndiye amekuwa akianzishwa na pia kupishana na Samatta pale timu hiyo inapofanya mabadiliko katika idadi kubwa ya mechi.

Mchezo wa mwisho ni wa juzi ugenini wa Mashindano ya Europa Conference League ambao PAOK iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudiwa Brendan Thomas akianza na kucheza kwa dakika 88 huku Samatta akishindwa kuwepo hata benchi.

AZIZ KI AFUNGUKA “UCHAWI” ULIOMFANYA ARUDI ‘MJINI’ NA YANGA MSIMU HUU… WIKIEND YA KIPUTE CHA ‘MIHELA’ INAANZA KESHO….KAMATA ODDS ZA USHINDI KUPITIA MERIDIANBET..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply