Habari za michezo
DIOUMBIA AIKALIA YANGA KOONI, WIKI MOJA BAADA YA KUREJEA NCHINI
Staff Desk
September 2, 2023
3:17 am
Kwa mujibu wa Goal Africa, aliyekuwa beki wa Yanga, Mamadou Doumbia ametoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa Yanga kumlipa stahiki zake.
Doumbia aliyerejea nchini wiki iliyopita ametishia kwenda kushitaki FIFA kama hatakamilishiwa malipo yake.
Doumbia raia wa Mali kwa sasa yuko nchini kwa takribani wiki ya pili ambapo ametishia kuwa atapeleka malalamiko FIFA na Yanga italazimika kumlipa hata gharama anazotumia sasa wakati akisubiri kulipwa stahiki zake.
Kinachofanywa na Doumbia ni kama ‘kuikomoa’ Yanga baada ya kuvunja mkataba wake mwezi uliopita huku mwenyewe akionekana kutoridhishwa na uamuzi huo.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.