Home Habari za michezo KISA MIQUISSONE KUPUNGUZA ‘UBONGE’…MBRAZILI SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA…

KISA MIQUISSONE KUPUNGUZA ‘UBONGE’…MBRAZILI SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA…

Habari za Simba

Kocha wa Simba Robertinho amesema amefurahishwa na kitendo cha winga Luis Miquissone kupungua uzito, akisema kurejea kwake kwenye kiwango na wepesi kutaiongezea kitu kizito timu yake huku pia akisubiri taarifa njema za kipa aliyekuwa majeruhi, Aishi Manula.

Kocha alisema Luis alirejeshwa Simba akiwa na uzito wa kilo 77, lakini hadi sasa jamaa amekata kilo nne na kubaki na 73 ambazo zimemrudisha kwenye wepesi na juzi akifunga bao lake kwenye mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya Kipanga.

Winga huyo ndiye aliyeitungua Al Ahly mara ya mwisho ilipovaana na Simba Kwa Mkapa kwenye mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2020-2021 kabla ya timu hiyo kumnunua mwishoni mwa msimu huo na kuitumikia kabla ya hivi karibu kuvunja mkataba na kurudia Msimbazi kuliamsha upya.

“Jambo zuri kuna wachezaji wetu wengine wameanza kuimarika angalia Miquissone (Luis) ni mchezaji mkubwa ambaye anajua kuamua mechi kubwa kama hizi sasa amepungua uzito anarudi kwa kasi kwenye kiwango chake, Inonga (Henock) amerejea pia tunasubiri kusikia taarifa njema kuhusu Manula (Aishi).”

Simba itacheza mchezo wa pili wa kirafiki leo Jumanne kwenye Uwanja wa MO Simba Arena uliopo Bunju B ikiwa ni hitaji la benchi la ufundi la timu hiyo likitaka kuwaweka tayari wachezaji kwa kiushindani kabla ya kuifuata Dynamos kwa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa itakayopigwa Sept 16.

SOMA NA HII  MABINGWA WOTE WA MASHINDANO YA CAF NI KUJICHOTEA MABILIONI YA PESA...SIMBA WAKIKAZA TU WAMO...